Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kikao chenye anwani "Ujumbe wa Karbala na sherehe ya ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran", kimefanyika katika mji wa Jacobabad, Sindh, huku kikihudhuriwa na shakhsia za kidini, kijamii na kisiasa.
Katika hafla hiyo, ushindi wa hivi karibuni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake, hasa Marekani, uliwekwa wazi, na ushindi huo ulitajwa kuwa ni matokeo ya subira, uvumilivu na imani ya mataifa huru, hasa taifa la Iran, watu wa Palestina na wanyonge wa Ghaza.
Katika kikao hicho, Hujjatul-Islām Maqsood Ali Domki, mjumbe mwandamizi wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan (Majlis Wahdat-e-Muslimeen), huku akirejea uongozi wenye hekima wa Ayatollah al-‘Uzmā Sayyid Ali Khamenei katika zama hizi, alieleza:
“Leo hii, Kiongozi wa Waislamu duniani, kwa kupata ilhamu kutokana na ujumbe wa Imam Hussein, amesimama kwa ujasiri dhidi ya ‘twaghut’ wa zama hizi – yaani Marekani na utawala wa Kizayuni. Msimamo wake wa kuwaunga mkono watu wanyonge wa Palestina umeleta aibu na kushindwa kwa utawala wa Kizayuni, jambo ambalo ni fahari kwa Umma wa Kiislamu.”
Akaongeza kwa kusisitiza:
“Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu si ushindi wa taifa la Iran pekee, bali ni mafanikio makubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu; ni alama ya imani, maarifa ya ndani na subira thabiti.”
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistan aliendelea kwa kusisitiza ujumbe wa kimataifa wa Imam Hussein (as), akisema:
“Mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Imam Hussein (as), si wa dhehebu au taifa fulani tu, bali ni kiongozi na mkombozi wa wanadamu wote. Kufahamu ujumbe wa Karbala kunawezekana tu kwa kutafakari kwa kina maneno na mwenendo wa vitendo vya Mtukufu huyo.”
Maoni yako